Search from various 영어 teachers...
zachariah getubo
Days of the week in swahili Siku za wiki Kuna siku saba katika juma moja. Jumapili huwa siku ya kwanza katika juma. Siku hii wakristo wengi duniani huenda kanisani.

Siku ya pili huwa ni Jumatatu. Ambapo watu hurejea kazini baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki. Kwa kiingereza siku hii hujulikana kama 'Monday'.

Siku ya tatu huwa ni Jumanne. Hapa wanadamu huchapa kazi kwa bidii kwa kuwa uchovu wa wikendi huwa umekwisha na hivyo wanatia bidii. 

Katikati mwa wiki kuna Jumatano. Katika lugha ya kiingereza siku hii hujulikana kama 'Wednesday'.

Alhamisi huwa siku ya tano katika wiki. Tayari uchovu wa binadamu unaanza kujitokeza hivyo anahitaji mapumziko. 

Ijumaa huwa ni siku ya sita. Pia siku hii huwa ya mwisho kazini katika juma zima. Walimwengu huanza kujitayarisha kwa ajili ya wikendi. 

Siku ya saba huwa Jumamosi. Mara nyingi binadamu huwa mchovu katika siku hii. Binadamu wengine huabudu mungu katika siku hii. 

2019년 1월 26일 오전 11:10

집에서 편안하게 언어를 배울 수 있는 기회를 놓치지 마세요. 경험 많은 강사진을 살펴보고 지금 바로 첫 수업을 신청하세요!