Berthod Vedasto
Sungura mjanja

For those who are interested in learning swahili language and those knowing a little swahili welcome. This is a good swahili story concerning a rabbit and lion. It is really enjoyable and pleasing. In swahili we say "sungura mjanja" meaning "a slick rabbit". Welcome all even if you don't know swahili. It is easy to learn swahili!!!!

Hapo zamani palikuwepo na simba aliyejulikana kama mfalme wa wanyama wote porini. Siku moja aliamua kumtembelea Sungura aliye julikana kuwa mwerevu na mjanja sana kule porini. Basi, simba alipofika nyumbani kwa Sungura mjanja, sungura akatoka akamkaribisha akae. Simba akakataa kukaka akamwambia,’ mie nina njaa kweli sijala siku ya tatu sasa, Swala na nyumbu ambao ndio chakula chetu ukoo wa kifalme wamegoma, wanasema tusubiri hadi mmoja wao afe ndio tule mzoga’. akaendelea Kumwambia sungura,  ‘mgomo huu umetushangaza sana familia ya kifalme na katika kikao chetu cha ikulu jana tumeamua kuwa kwa sababu nyie mko jirani na ni wengi basi nyie ndo mtakuwa chakula chetu’.

Sungura wakati huo alikuwa anamsikiliza kwa makini sana. Baada ya maelezo marefu kutoka kwa simba kuhusu maamuzi ya familia ya kifalme, sungura akamwambia, ‘lakini mfalme kwa nini uhangaike kutafuta chakula wakati mnazaa vitoto vingi hivyo?’, ‘Sie sungura tuko wadogo kama vile vitoto vyenu na hata nyama ya vitoto vyenu ni tamu kuliko yetu’. Simba baada ya kusikiliza kwa makini akamshukuru Sungura kwa ushauri wake akarudi nyumbani.  Alivyofika tu nyumbani akaanza kukamata vitoto vyake na kuvila, alipokuja mama wa vitoto vile akakuta vitano vimeshaliwa tayari. Simba jike akaanza kugomba na kupigana na mumewe. Baada ya ugomvi simba jike akamuuliza dume kwa nini umefanya kitendo kibaya namna hii? Simba dume akajibu, ‘ ni shauri ya sungura, kaniambia watoto wetu ni watamu kuliko wao’.

Simba jike alikasirika sana akamwendea sungura mbio, Sungura kuona hivo akatoka mkuku. Wakaanza kufukuzana hadi kwenye kichuguu, sungura akaingia kwenye shimo. Simba akakamata mkia akaanza kuvuta, Sungura alipoona kashikwa mkia akamwambia simba,’ mbona unaacha kushika mkia unashika mzizi wa mti?’. Simba kusikia hivyo akaachia mkia wa sungura akashika mzizi wa mti akidhani ndio mkia wa sungura. Sungura akamwambia shikilia hapo, vuta kwa nguvu. Sungura akajichimbia chini zaidi na simba hakuambulia kitu, akarudi nyumbani kwa huzuni.

Apr 30, 2018 2:41 PM
Comments · 3
1
Thank you. I don't understand the story yet. But it will be fun and challenging to try an make sense of it.
June 1, 2018
1
Asante sana Berthod! 
May 6, 2018

hadithi nzuri, nimefurahi kuisoma. 


Umetumia maneno machache sitambui, kama "nyie mko" na "sie." Tafsiri maneno haya, tafadhali?

June 17, 2018