Search from various 영어 teachers...
[삭제됨]
Chakula kilicho pichani kinajulikana kama chapati nchini Kenya. Hutengenezwa kwa mchanganyiko wa unga wa ngano, sukari, chumvi, mafuta/siagi. Ni mkate ulioshikamana baada ya kukandamizwa katika sehemu bapa. Mkate huu huwa wa mviringo na unakaangwa kwa mafuta. Unaweza kutowelewa kwa nyama ya ng'ombe/mbuzi iliyo na supu, mboga za majani zilizokaangwa, maharage ya nazi, mchuzi wa viazi na mbaazi au samaki aliyeandaliwa kwa supu iliyotiwa viungo. Wakati mwingine huliwa kwa vinywaji vya chai, kahawa au sharubati. Chapati ni chakula kitamu sana. Kando na kupikwa nyumbani, huuzwa mikahawani pia. Furahia mlo wa chapati utembeapo Afrika Mashariki, haswa Kenya, Tanzania na Uganda. Maswali ✨Chapati hupikwa kutumia viungo vipi?(1.) ✨Chakula hiki hupatikana nyumbani na wapi kwingine? (2.) ✨Chapati huwa na umbo gani? (3.) ✨Je, ungependa kutowelea Chapati kwa? (4.) ✨Nchi zipi zilizotajwa ambazo unaweza ukapata Chapati kwa urahisi? (5.)
2024년 8월 21일 오후 1:22

집에서 편안하게 언어를 배울 수 있는 기회를 놓치지 마세요. 경험 많은 강사진을 살펴보고 지금 바로 첫 수업을 신청하세요!