Rebekah
Mazungumzo ya kiswahili cha kiwango cha juu

Mambo vipi, wanafunzi na wasemaji wa Kiswahili? Natafuta watu wanaopenda kuzungumza kiswahili cha kiwango cha juu--ama wanafunzi wengine ambao wamewahi kusoma lugha muda mrefu au wasemaji wa kiswahili kama lugha mama (native speakers). Mimi mwenyewe nimebahatika kukaa Afrika Mashariki miesi 8 hivi kwa jumla, na nimesoma lugha darasani tangu 2012. Labda kuna mwalimu ambaye angependa changamoto ya kuandaa kozi ya kiwango cha juu? Au wasemaji wengine wanaopenda kutumia lugha yao? Kwa bahati mbaya, sina pesa ya kulipia masomo, lakini ningefurahi kukusaidia na masomo ya kiingereza au kiitaliano (hata kama kiitaliano changu si kizuri sana).

Pia, natafuta msemaji wa kisukuma. Ukiwa msukuma, tafadhali nijulishe!

4 gen 2017 20:49
Commenti · 4
2

Kiswahili chako ni kizuri sana. Nafurahi sana kuona umejifunza Kiswahili mpaka hatua hiyo uliyofikia, hongera sana. Mimi ni mswahili. Na ningependa tufahamiane na unisaidie kiingereza changu hapo baadae.

Wewe ni Mmarekani wa kwanza kusikia unataka kujua kisukuma, ni changamoto kidogo kujifunza lugha za makabila za Tanzania kwa kuwa siku hizi hazipewi vipaumbele na hamna vitabu wala video za kukusaidia ila natumai ukipata Msukuma atakusaidia.

Swali la kizushi: Kwanini kisukuma? na sio labda kichaga au kihaya?


16 gennaio 2017
2
Haha.halo. Mimi ni mtanzania na ningependa kukusaidia kwenye lugha ya kiswahili lakini siwezi sema mimi ni mtaalamu wa lugha. Inafurahisha kujua ungependa kujua kisukuma
11 gennaio 2017
1

Asanteni Ian na Doni! Nimefurahi kupata majibu yenu. 

Doni nakubali na wewe--lugha za makabila hazapewi vipaumbele kabisa kwa bahati mbaya. Lakini bado watu wanazitumia nyumbani. Mimi ni mwanaanthropolojia, yaani nafanya utafiti wa sayansi ya jamii. Utafiti wangu hufanyiwa Mwanza na Shinyanga, kwa hiyo nataka niweze kuongea na wenyeji wa huko. Mbeleni nataka kujifunza lugha za makabila mengine. Wewe unaweza kuongea kilugha? 

16 gennaio 2017

Ningependa kushiriki mazungumzo haya pia! Mimi ni mgeni kwa italki kwa hiyo sijui itakavyofanyika-- Kwa skype labda? 

Nimetembelea Kenya mara kadhaa (nadhani nimekaa kama miezi saba kwa jumla?), nikajaribu kuzifunza Kikuyu lakini sijaweza kuendelea juu ya ukosefu wa kitabu, video, n.k., mlivyotaja. Nina kitabu kimoja cha kale nisichotumia kwa sababu niliambiwa maneno mengi ndani chake hayatumiki siku hizi, au maana yake yamebadilika. Kwa mfano, sana sana kitabu hicho kilitumia kitenza "gwata," iliyosemekana kumaanisha "shika" na rafiki yangu alisema "gwata" siku hizi ni "baka"! 

Vipaumbele ni nini?

28 luglio 2017