Search from various Tiếng Anh teachers...
[Người dùng đã hủy tài khoản]
Sima ni chakula kinachotambulika zaidi nchini Kenya.
Sima pia huitwa ugali.
Hutayarishwa kwa kusonga unga wa mtama, mahindi au muhogo kwenye maji moto yaliyochemka.
Sima huliwa kwa kitoweo cha nyama ama mboga za majani aghalabu.
Uwapo na ugali na mboga, ijapokuwa mboga zaweza kuwa kidogo, utaona kama umekula vyema, Sima yajua kucheza na akili aisee 😁
Ujapo Kenya, usichelee kujaribu mlo huu uwezao kuliwa wakati wowote.
0:44
8 Thg 08 2024 13:06



